Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanajeshi wa serikali DR Congo wakamatwa kwa ubakaji

Wanajeshi wa serikali DR Congo wakamatwa kwa ubakaji

Wanajeshi takribani 11 wa jeshi la serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamekamatwa wakishukiwa kujihusisha na ubakaji na uporaji kwa mujibu wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO.

MONUSCO inasema watu hao akiwemo afisa wa jeshi wanashutumiwa kuwabaka wanawake 13 kwenye mji wa Fizi Mashariki mwa Congo mapema mwezi huu. Tarehe nane mwezi huu mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukatili wa kimapenzi Margot Wallstrom aliitaka serikali ya Congo DRC kufanya uchunguzi wa kina haraka kuhusu taarifa za ubakaji huo uliotokea Fizi jimbo la Kivu ya Kusini na kuwafikisha wahusika kwenye mkono wa sheria.