Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP inaongeza msaada kwa wakimbizi wa Ivory Coast

WFP inaongeza msaada kwa wakimbizi wa Ivory Coast

Operesheni za shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP za kugawa msaada wa chakula kwa wakimbizi wa Ivory Coast walioko Liberia zimeingia katika hatua mpya.

Hatua hiyo ni kuanza usambazaji wa jumla wa chakula ikiwalenga wakimbizi 22,507 walioko katika vijiji 23 vya mpakani nchini Liberia ambavyo vinawahifadhi wakimbizi hao wa Ivory Coast. Jason Nyakundi na ripoti kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)

Wakati huohuo shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema mgogoro wa kisiasa unaondelea nchini Ivory Coast unatishia maisha ya mamilioni ya watu. Limeongeza kuwa ingawa mashirika ya misaada yanajitahidi kwa kila njia kufikisha msaada kwa wanaouhitaji haraka hususan wanawake, watoto na wazee, ni muhimu mazingira mazuri ya kufanikisha hilo yawepo.