UM walaani bughudha dhidi ya walinda amani wake Ivory Coast

UM walaani bughudha dhidi ya walinda amani wake Ivory Coast

Umoja wa Mataifa umelaani bughudha waliyofanyiwa wanajeshi wake wa kulinda amani nchini Ivory Coast UNOCI.

Bughudha hiyo imefanywa na wanajeshi wanaomuunga mkono Laurent Gbagbo mjini Abidjan.

Kwa mujibu wa UNOCI msukosuko dhidi ya wanajeshi wake umefanyika siku moja baada ya majeshi yanayomuunga mkono Bwana Gbagbo kuweka vizuizi na kupora msafara wao ukielekea kwenye hotel ya Golf kupeleka mahitaji muhimu.

Hotel hiyo inatumika kama makao makuu ya Alassane Ouattara ambaye anatambulika kama mshindi halali wa uchaguzi wa duru ya pili ya uraisi iliyofanyika mwezi Novemba mwaka jana nchini Ivory Coast.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa taarifa pia kulaani tukio hilo lililofanyika jana usiku kwenye eneo la Abobo mjini Abijan.Walinda amani hao walifyatuliwa risasi na wakajibu mashambulizi na kwenye purukushani hiyo wanajeshi watatu wa UNOCI walijeruhiwa kidogo.