Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ataka utulivu baada ya serikali kusambaratika Lebanon

Ban ataka utulivu baada ya serikali kusambaratika Lebanon

Serikali ya Lebanon leo imesambaratika baada ya mawaziri 11 kutoka vuguvugu la Kishia la Hizbollah na washirika wao kujiuzulu .

Kufuatia hatua hiyo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anafuatilia kwa karibu hali inavyoendelea kubadilika kwa haraka. Ban amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuna utulivu unadumishwa, pia ametoa wito wa kuendelea

kuwepo na mazungumzo katika pande zote na kuheshimu katiba na sheria za Lebanon. Ban amerea kauali yake ya Umoja wa Mataifa kuisaidia kuhakikisha utendaji huru wa mahakama maalumu ya Lebanon.