Skip to main content

Msaada wa Japan kwa WFP utafaidi mataifa 20

Msaada wa Japan kwa WFP utafaidi mataifa 20

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limekaribisha msaada wa dola milioni 196 kutoka kwa serikali ya Japan ukiwa ndio msaada mkubwa zaidi kuwahi kutolewa na nchi moja kwa shirika hilo.

Inasema kuwa misaada ya kifedha kutoka Japan inayosadia programu za chakula za WFP nchini Pakistan na Afghanistan ni ishara ya jitihada za Japan za kuleta amani katika eneo hilo. Barani afrika msaada huo utasaidia program kwenye nchi 17 ambapo watu wanahitaji zaidi msaada wa chakula kufuatia kuwepo kwa mizozo na majanga mengine yakiwemo ukame na mafuriko.