Skip to main content

Matokeo ya kura ya maoni ni hisia za wananchi:Mkapa

Matokeo ya kura ya maoni ni hisia za wananchi:Mkapa

Mkuu wa jopo la Umoja wa Mataifa lililiteuliwa kuangalia kura ya maoni kusinu mwa Sudan na rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa amesema kuwa kura hiyo itaonyesha hisia kamili za wapiga kura.

Mkapa ni mmoja wa wanachama watatu wa jopo hilo ambao wamekuwa wakizuru vituo vya kupigia kura kusini mwa Sudan ambapo walikutana na wasimamizi wa uchaguzi huo na wapiga kura kwenye majimbo ya South Darfur, Upper Nile na Bahr el-Ghazal.

Rais huyo wa zamani wa Tanzania amesema kuwa ana matumani kuwa wakati zoezi la kuhesabiwa kwa kura litakapoanza kutakuwa na utulivu na uwazi sawia na unaoshuhudiwa wakati wa kupiga kura.