Asilimia 60 wajitokeza katika kura ya maoni Sudan
Taarifa kutoka Juba mji mkuu wa Sudan Kusini zinakinukuu chama tawala cha eneo hilo kusema asilimia 60 ya wapiga kura inayotakiwa ili kuhalalisha kura hiyo ya maoni imetimia.
Hatua hiyo imefikiwa katika siku ya tatu ya upigaji kura. Waasi wa zamani wa chama cha Sudan Peoples Liberation Movement SPLM wametoa makadirio yao ya mafanikio ya kura hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa inasimamiwa na Umoja wa Mataifa, lakini yatahitaji kudhibitishwa rasmi na tume ya kuara ya maoni ya Sudan Kusini ambayo ndio imeandaa mchakato wa wiki nzima wa kura hiyo.
Siku ya mwisho ya upigaji kura ni Jumamosi Januari . wakati huohuo shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO limesema usalama wa chakula Sudan Kusini umeimarika kwa mwaka 2010, na idadi ya watu wanaotegemea msaada wa chakula katika eneo hilo imepungua.
Hata hivyo FAO inasema hatma ya usalama huo itategemea sana hali itakayojitokeza baada ya kura ya maoni. Jason Nyakundi na ripoti kamili.
(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)