Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lazima tuongeze juhudi kuisaidia Haiti:UNESCO

Lazima tuongeze juhudi kuisaidia Haiti:UNESCO

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la sayansi, elimu na utamaduni Irina Bokova ameitolea wito jumuiya ya kimataifa kutekeleza ahadi zake za kuongeza juhudi na msaada kwa nchi ya Haiti.

Amesema hali ya Haiti inaendelea kuwa mbaya, watu takriban milioni moja bado hawana makazi ya kudumu na wanaishi katika mazingira magumu.Ameongeza kuwa ujenzi mpya unaenda polepole na msaada ulioombwa kwa ajili ya nchi hiyo ni shemu ndogo tuu ndio iliyopatikana.

Serikali na jumuiya za kijamii Haiti na kwingineko lazima zioneze msaada kuinusuru Haiti amesema Bi Bokova kwani nchi hiyo inachohitaji hivi sasa ni suluhu ya muda mrefu ambayo ni ujenzi mpya.