Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM utaendelea kuisaidia Haiti katika ujenzi mpya: Ban

UM utaendelea kuisaidia Haiti katika ujenzi mpya: Ban

Leo katika kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kutokea tetemeko la ardhi nchini Haiti Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameelezea mshikamano wake kwa watu wa Haiti na wote walioathirika bibaya na tetemeko hilo.

Katika taarifa yake maalumu Ban amesema Haiti imekumbwa na pigo kubwa lisilielezeka, tetemeko siku hiyo Januari 2 mwaka 2010 watu zaidi ya laki mbili waliuawa, zaidi ya laki tatu kujeruhiwa na kuwaacha milioni 2.3 bila makazi.

Ameongeza kuwa serikali ilipoteza wafanyakazi wengi huku miundombinu ya nchi hiyo ikisambaratika vibaya. Wafanyakazi 102 wa Umoja wa Mataifa pia walipoteza maisha katika tetemeko hilo na Umoja wa Mataifa daiana utawakumbuka.

Ban amerejea kauli yake kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kuisaidia serikali ya Haiti na watu wake katika kukabili changamoto za ujenzi mpya.