Leo January 12 mwaka 2011 ni mwaka mmoja tangu Haiti kukumbwa na tetemeko kubwa la ardhi

12 Januari 2011

Tarehe 12 Januari mwaka 2010, ikiwa sasa ni mwaka mmoja kambili, Haiti na dunia ilijikuta ikipigwa na butwaa baada ya tetemeko kubwa kuikumba Haiti nchi iliyoko kwenye visiwa vya Carebean.

Tangu tetemeko hilo kwa Haiti mwaka 210 ukawa ni wa maafa na changamoto kubwa katika historia yake. Tetemeko hilo la Januari 12 lililkatili maisha ya watu na kusababisha uharibifu mkubwa. Watu takribani 250,000 wanakadiriwa kufa na wengine 300,000 kujeruhiwa huku milioni 1.3 waliachwa bila makazi na miundombinu ya nchi hiyo kusambaratika.

Kwa Umoja wa Mataifa 2010 pia ulikuwa mwaka wa changamoto , haikupoteza tuu wafanyakazi wake na uongozi wao kwenye mpango wake nchini humo MINUSTAH, lakini uliongoza msaada wa kibinadamu baada ya tetemeko hilo na kuifanya dunia kuelekeza nguvu zake katika kuisaidia Haiti.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, alizuru mji ulioathirika vibaya wa Port-au-Prince. Sikiliza kipindi hiki maalumu.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter