Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa nyumba bado ni tatizo kubwa katika ujenzi mpya Haiti: IOM

Ukosefu wa nyumba bado ni tatizo kubwa katika ujenzi mpya Haiti: IOM

Karibu Wahaiti 810,000 bado wanaishi kwenye mahema kwenye makambi ya muda mwaka mmoja baada ya tetemeko la ardhi limesema shirika la uhamiaji la kimataifa IOM.

Kwa mujibu wa shirika hilo hata hivyo idadi ni ndogo ikilinganishwa na milioni 1.5 ambao waliwekwa kwenye makambi ya muda mara tuu baada ya tetemeko.

Msemaji wa IOM mjini Geneva Jemini Pandya amesema kuwarejesha kwenye nyumba zao waathirika wa tetemeko la mwaka jana ni ajenda muhimu katika mipango ya muda mrefu ya ujenzi mpya wa Haiti, lakini kuna vikwazo vingi na huenda ikachukua muda mrefu.

(SAUTI YA JEMINI PANDYA)

IOM inasema shughuli za kuratibu masuala ya kwenye makambi zimekuwa zikikosa ufadhili wa kutosha, ambapo hadi sasa zimepokea chini ya nusu ya fedha zinazohitajika.