China ichunguze kifo cha mwandishi habari:UNESCO

10 Januari 2011

Serikali ya Uchina imetakiwa na mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la sayansi, elimu na utamaduni UNESCO kuchunguza kifo cha mwandishi habari wa Kichina Sun Hongjie.

Hongjie alikuwa akifanya kazi kama ripota kwenye gazeti la Beijing la Chenbao. Sun Hongjie amearifiwa kufariki dunia kutokana na majeraha kichwani kwenye hospitali ya mji wa Kuitun jimbo la Kaskazini Magharibi la Xinjiang tarehe 28 Desemba mwaka jana.

Mwandishi huyo amearifiwa kushambuliwa usiku wa Desemba 18 na kundi la watu sita kwenye eneo la ujenzi ambako alikuwa na miaydi ya kukutana na mtu wa kumpa habari. Bi Irina Bokova mkuu wa UNESCo amesema kutokana na mazingira ya shambulio lenyewe anautaka uongozi wa Uchina kuchunguza kwa kina uhalifu huo na kuwafikisha wahusika kwenye mkono wa sheria.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter