Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yaendelea kusaidia kilimo nchini Haiti

FAO yaendelea kusaidia kilimo nchini Haiti

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO, limesema limefanikiwa kutoa vifaa kama mbegu, mbolea pamoja na pembejeo nyingine kwa ziadi ya wananchi milioni mbili wa Haiti, ambao waliokumbwa na mafuriko mabaya yaliyoharibu mfumo mzima wa kilimo.

Wananchi hao sasa wanaanza kurejea upya kwenye shughuli za kilimo, baada ya kupita kipindi cha mwaka mmoja tangu kutokea kwa mafuriko hayo.

FAO inakadiria kuwa nusu ya wananchi wa Haiti wanaishi kwenye maeneo ya vijijini ambako wanajishughulisha na shughuli mbalimbali zinazohusiana na kilimo. Kilimo ni sekta muhimu nchini Haiti kwani inaajiri idadi kubwa ya watu na imekuwa ikichangia pato la taifa kwa asilimia 26.