Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa haki za binadamu azuru India

Mtaalamu wa haki za binadamu azuru India

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na kuchunguza hali watetesi wa haki za binadamu Margaret Sekaggya ameanza ziara yake ya siku 11 nchini India iliyo na lengo la kuchunguza hali ya watetesi wa haki za binidamu nchini India na kutafuta njia za kushirikiana na serikali ya nchi hiyo.

Mjumbe huyo anatarajiwa kukutana na maafisa wa serikali, mashirika ya umma , waandishi wa habari na waakilishi wa mshirika ya Umoja wa Mataifa. Mjumbe huyo atayazuru majimbo ya Gujarat, Jammu na Kashmir ,Orissa na West Bengal na kufanya mashauriano na watetesi wa haki za binadamu mjini Delhi.

Baadaye atatafanya mkutano na waandishi wa habari tarehe 21 mwezi huu wakati wa kumalizika kwa ziara yake huku ripoti kuhusu ziara hiyo ikitarajiwa kuwasilishwa kwenye baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa mwaka 2012.