Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanafunzi Haiti wakabiliwa na tisho la kipindupindu:OCHA

Wanafunzi Haiti wakabiliwa na tisho la kipindupindu:OCHA

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA linasema kuwa karibu watoto milioni 2.2 nchini Haiti wanakabiliwa na hatari ya kuambukizwa ugongwa wa kipindupindu.

Hali  hali hiyo  huenda ikasababishwa na uhaba wa maji safi na mazingira machafu shuleni. Kulingana na ripoti yake ya kila wiki kuhusu ugonjwa wa kipindupindu nchini Haiti , OCHA inasema kuwa huduma za kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo kama vile kuwapa mafunzo walimu na kugawa vifaa vya kunawa mikono havitoshi kusaidia kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo kwenye mashule . Flora Nducha anaripoti

(RIPOTI YA FLORA NDUCHA)

Ripoti inasema visa vya kipindupindu bado vinaripotiwa katika vituo vya kulelea watoto na vituo vya watoto yatima licha ya fedha kubwa ziolizowekezwa katika kutoa mafunzo na miradi ya kuelimisha. OCHA inaonyesha kwamba kuna pigo kubwa katika juhudi za kuzuia kusambaa kwa kipindupindu.

 Ombi la Umoja wa Mataifa la dola milioni 174 kusaidia kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo Haiti hadi sasa wamepokea dola milioni 44 tuu. Na wakati shule zimefunguliwa kwa msimu mwingine OCHA inasema juhudi zinafanyika kuzifikia shule takribani 10,000 na kuzipa vifaa vya kudhibiti ugonjwa huo zikiwemo sabuni za kunawia mikono.

Utoaji taarifa kupitia vituo vya radio, na mafunzo kwa waalimu na viongozi wa jamii kuhusu kuzuia kusambaa kipindupindu yataongezwa. Watu karibu 37000 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo tangu ulipozuka Haiti.