Maelfu ya raia wa Sudan Kusini wajitokeza kupiga kura ya amaoni inayoungwa mkono na UM

Maelfu ya raia wa Sudan Kusini wajitokeza kupiga kura ya amaoni inayoungwa mkono na UM

Huku kura maoni Sudan kusini ikiingia siku yake ya pili hii leo kumeshudiwa idadi mkubwa ya wapiga kura na milolongo mirefu kwenye uchaguzi ulio na karibu wa wapiga kura milioni 4 waliojiandikisha.

Maafisa wa tume ya uchaguzi kusini mwa Sudan wametaja siku ya kwanza ya kura hiyo kuwa iliyofanikiwa huku mashirika yakiwemo ya Umoja wa Mataifa na vikosi vya kulinda amani wakitoa usaidizi wa kiufundi na usafirishaji. Jobo linaloangalia kura hiyo chini ya uongozi wa rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa linajitahidi kuhakikisha kuwa zoezi hilo limeendeshwa kwa njia ya haki , usawa na huru.

Hata hivyo vyombo vya habari vinaripoti kuwa zaidi ya watu 20 wameuawa kwenye eneo lenye utajiri wa mafuta na linalozozaniwa la Abyei kwa muda wa siku chache zilizopita kati ya jamii ya kiarabu ya Misseriya na jamii ya Ngok Dinka.

Darin Farrant ni mmoja wa wajumbe wa jopo la Umoja wa Mataifa lililoteuliwa na Katibu Mkuu Ban Ki-moon kuangalia kura hiyo ya maoni.

(SAUTI YA DARIN FARRANT)

Mkatanba wa amani wa mwaka 2005 ndio ulimaliza vita vya miongo miwili katika ya Sudan kaskazini na Kusini ambapo watu milioni 1.5 waliuawa. Kura hiyo ni moja ya makubaliano ya mkataba huo na huenda ikasababisha kugawanywa mara mbili kwa taifa la Sudan.