Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuongeza vikosi vyake Ivory Coast: Le Roy

UM kuongeza vikosi vyake Ivory Coast: Le Roy

Umoja wa Mataifa unatazamia kuongeza idadi ya askari wake wa kulinda amani nchini Côte d\'Ivoire kwa lengo la kuimalisha hali ya usalama katika wakati ambapo rais aliyemaliza muda wake akiendelea kutia ngumu kukabidhi madaraka.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, anakusudia kuliomba baraza la usalama kutuma kati ya askari 1000 ama 2000 ili kuongeza nguvu kwenye vikosi vya umoja huo vilivyoko nchini humo. Vikosi hivyo vitakavyoongezwa, vinatazamiwa pia kuendesha operesheni ya amani kwenye maeneo ya jirani ikiwemo Liberia.

Hali ya usalama nchini Ivory Cost bado imeendelea kuwa tete na taarifa zimesema kuwa idadi ya watu wanaopoteza maisha imeendelea kuongezeka