Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaanza kuweka mipango kuwasaidia wakimbizi wa Zimbabwe

IOM yaanza kuweka mipango kuwasaidia wakimbizi wa Zimbabwe

Shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa limeanza kuandaa huduma za dharura ya misaada ya kibinadamu kwa ajili ya wakimbizi wa Zimbabwe waliokimbilia nchini Afrika Kusin ambao wanaweza kulazimika kurejea nyumbani mwaka huu.

Mamia kwa maelfu ya wakimbizi wa Kizimbabwe ambao walitorokea nchini Afrika Kusin kinyume sha sheria wanakabiliwa na wakati mgumu wa kurejeshwa nyumbani kufuatia kukamilika kwa msamaha uliowapa fursa ya kusalia nchini humo kwa muda mchache.

Zaidi ya wazimbabwe 276,000 walisajiliwa kufutia kampeni iliyoaendeshwa na serikali ya afrika kusin mwaka uliopita, lakini takwimu zinaonyesha kuna raia wegine zaidi ya milioni moja ambao wanaishi kinyume cha sheria.

Ili kukabiliana na wimbo hilo linaloweza kujitokeza shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa imeanza kuweka mikakati ya utoaji wa misaada ya kisamaria.