Huduma za WFP nchini Iraq zapata ufadhili wa dola milioni 1.5

7 Januari 2011

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limepokea dola milioni 1.5 ambazo litatumia kufadhili mpango wa kuchangisha fedha zitakazotumika kugharamia oparesheni zake nchini Iraq.

Mpango huo una lengo kuchangisha fedhaa ambazo pia zitatumika kusafirisha mahitaji muhimu ya kibinadamu kupitia kwa njia ya ndege kote nchini Iraq.

Huduma za usafirishaji wa ndege zilizo nchini Iraq kwa sasa hazitekelezi ipasavyo majukumu ya Umoja wa Mataifa ambapo mara nyingi huwa zinakumbwa na matatizo ya kimitambo , kuchelewa na kuwepo kwa uhaba wa ndege.

Mara nyingi pia usafirishaji wa misaada ya kibinadamu unakabiliwa na masuala ya usalama na kuchelewa hali ambayo imechangiwa kuondoka kwa wanajeshi wa Marekani nchini Iraq ambao mara nyingo ndege zao zilikuwa zikitumika kusafisha misaada kama hiyo.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud