Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yapinga Ugiriki kujenga uzio kwenye mpaka na Uturuki

UNHCR yapinga Ugiriki kujenga uzio kwenye mpaka na Uturuki

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limeelezea hisia zake kuhusiana na tangazo la serikali ya Ugiriki kuwa itajenga ua wenye umbali wa kilomita 12 kwenye mpaka wake na Uturuki .

UNHCR inasema kuwa baadhi ya watu wanaovuka mpaka kupitia uturuki kwenda Ulaya wanakimbia ghasia na dhuluma na hivyo kuchukua hatua kama hizo za kuwazuia wakimbizi sio vyema.

UNHCR inasema kuwa ujenzi wa ua mara nyingi si suluhisho la uhamiaji na huenda kukachangia kwa watafuta hifadhi kubuni mbinu tofauti zilizo hatari kufika sehemu salama suala ambalo mara nyingi husababisha wakimbizi wengi kujipata mikononi mwa walanguzi wa binadamu.