Liberia ichukue hatua kuzuia uuzaji haramu wa almasi:UM

7 Januari 2011

Umoja wa Mataifa umesema kuwa Liberia nchi ambayo wakati mmoja ilikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe imepiga hatua katika kukabilina na biashara haramu ya madini ya risasi, mbao na raslimali zingine ambapo pesa zinatokana na biashara hiyo zimetumika kufadhili vita katika eneo la afrika magharibi.

Kulingana na jopo la wataalamu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Liberia ni kuwa taifa hilo linajikokota katika kuchukua hatua zifaazo kulingana na makubaliano ya Kimberley ya kuzua madini ya Almasi yanayotoka kwenye sehemu zinazokumbwa na mizozo.

Madini hayo yamekuwa chanzo kikuuu cha ukosefu wa utulivu barani afrika. Jopo hilo lililobuniwa mwaka 2007 limeitaka Liberia kuwa makini zaidi na kudhibiti uchimbaji na uuzaji wa madini ya Almasi ili kuzuia madini haramu kuingia kwenye madini yaliyo halali.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter