Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OCHA na UNEP waitaka serikali ya Nigeria kuzuia kusambaa kwa sumu

OCHA na UNEP waitaka serikali ya Nigeria kuzuia kusambaa kwa sumu

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP wameitolea wito serikali ya Nigeria kuzuaia kusambaa zaidi kwa sumu Kaskazini mwa nchi hiyo.

Ripoti ya pamoja iliyotolewa na mashirika hayo imependekeza kuchukuliwa hatua za kudhibiti uzalishaji wa chuma katika maeneo nyeti hasa kama vyanzo vya maji ambayo yanatumiwa na watu na mifugo kwa kunywa na matumizi mengine. Jason Nyakundi anaripoti.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)