Skip to main content

Haiti bado ina safari ndefu kurejea hali ya kawaida baada ya tetemeko:UNICEF

Haiti bado ina safari ndefu kurejea hali ya kawaida baada ya tetemeko:UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema mwaka mmoja baada ya tetemeko la ardhi la Januari 12 kuikumba Haiti,watoto milioni 4 bado wanakabiliwa na hali mbaya.

Shirika hilo linasema watoto hao wanakabiliwa na changamoto ya kukosa maji safi ambayo ni huduma muhimu, usafi, huduma za afya, elimu, kulindwa kutokana na maradhi, wananyonywa, na wanaendelea kuishi katika mazingira duni.

UNICEF inasema hadi leo hii zaidi ya watu milioni moja,ambapo takribani 380,000 kati yao ni watoto bado wanaishi katika makambi ya muda. Hata hivyo shirika hilo linasema jumuiya ya kimataifa imejitahidi kuokoa maisha ya mamilioni ya watu licha ya changamoto wanazokabiliana nazo kama anavyofafanua msemaji wa UNICEF Marixie Mercado.

(SAUTI YA MERXIE MERCADO)

Ameongeza kuwa watoto milioni 2 wamepata chanjo, kina mama zaidi ya 50,000 wameelimishwa kuepuka utapia mlo kwa watoto na watoto 720,000 wamerejea shuleni huku wengine 1300 wameunganishwa na familia zao.