Ukame ulioikumba Somalia unatia hofu kwa maisha ya watu:UM
Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia Bwana Mark Bowden ameelezea hofu yake kuhusu hali ya ukame iliyoikumba Somalia.
Mwaka 2010 ulighubikwa na uhaba wa mvua katika maeneo mengi ya Somalia na kwa sababu mavuno ya nchi hiyo yanategemea sana mvua hali ya maisha ya watu itazidi kuzorota katika miezi ijayo amesema bwana Bowden.
Watu milioni mbili tayari wanategemea msaada wa dharura na ukame utaongeza idadi hiyo mara dufu. Bwana Bowden ameilezea changamoto inayokabili jumuiya ya kimataifa kufikia maeneo ya Kusini na Katikati mwa Somalia yaliyoathirika kuwa ni kubwa.
Elizabeth Byrs ni msemaji wa shirika la Umoja wa mataifa la kuratibu masuala ya kibidamu OCHA anathibitisha kauli ya Bowden
(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)