Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya wakimbizi wa Ivory Coast waendelea kuingia Liberia:UNHCR

Maelfu ya wakimbizi wa Ivory Coast waendelea kuingia Liberia:UNHCR

Wakati mvutano wa kisiasa bado kupatiwa suluhu nchini Ivory Coast maelfu ya watu waendelea kukimbilia nchi jirani ya Liberia wakihofia usalama wao.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema tangu kuzuka machafuko Novemba mwaka jana wakimbizi 23,000 wameingia Liberia kwa idadi ya takribani 500 kwa siku.

Wakimbizi wengi bado wanahifadhiwa na familia za wenyeji na ujenzi wa kambi mpya jimboni Nimba kuwahifadhi wakimbizi hao bado haijaanza. UNHCR inasema sababu kuwa ni kwamba bado haijapata vibali muhimu ili kuanza ujenzi huo. Kwa sasa UNHCR na shirika la mpango wa chakula duniani WFP wanapanga kuanza ugawaji mkubwa wa chakula kwa wakimbizi hao wiki ijayo.