Kusini mwa Afrika waongezeka vita dhidi ya ukatili:UNODC

6 Januari 2011

Katika juhudi za kusaidia vyombo vya sheria Kusini mwa Afrika kukabiliana na ukatili wa kijinsia ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC leo imesema imezindua muongozo na muhula wa mafunzo ili kuimarisha uwezo wa majeshi ya polisi katika kanda hiyo kukabiliana na ukatili huo.

Kwa kupitia mpango huo UNODC inashirikiana na maafisa wa serikali na jumuiya za Botswana, Lesotho, Msumbiji, Namibia, Afrika ya Kusini na Zimbabwe kuunga mkono utekelezaji wa sheria na mifumo ya kitaifa ya kupambana na uhalifu ili kupambana na ukatili dhidi ya wanawake.

Muungozo huo umetayrishwa maalumu kwa watu kama polisi na unasaidia kufafanua kuhusu ukatili dhidi ya wanawake kwa kutoa mtazamo wa mila na viwango, lakini pia unatoa maelekezo ya jinsi ya kuingilia kusitisha ukatili huo. Zaidi ya hayo unajikita katika jinsi ya kufanya uchunguzi wa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake, machakato ambao unahitaji unyeti wa hali ya juu.

Na muhula wa mafunzo umeandaliwa ili kuwaelmisha raia na jeshi la polisi mbinu wanazohitaji kukabiliana na ukatili huo bila kuzusha tafrani, hasa wanapogusia mahusiano ya ndani ya watu. UNODC pia inafanya kazi na jamii za afrika ya Kusini kutoa msaada kwa waathirika wa ukatili dhidi ya wanawake.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter