Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usalama ni jambo linaloendelea kutia hofu Darfur:UM

Usalama ni jambo linaloendelea kutia hofu Darfur:UM

Usalama unasalia kuwa jambo linalopewa kipaumbele cha kwanza na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika Darfur UNAMID amesema mkuu wa mpango huo Ibrahim Gambari.

Akianinisha masuala yanayopewa kipaumbele na UNAMID kwa mwaka huu wa 2011 amesema mpango huo utaendelea kuhakikisha kunakuwa na mazingira mazuri ikiwepo kuwalinda raia. Bwana Gambari amewataka wafanyakazi wa UNAMID kuendel;ea kuunga mkono amani ya Darfur na mchakato wa kisiasa, na kupata suluhu ya kudumua itakayojumuisha wote ambayo itashughulikia kiini cha mgogoro wa Darfur.

Ameongeza hilo ni pamoja na kuunga mkono na kusaidia kurejea kwa hiyari kwa wakimbizi wa ndani na wakimbizi wa kawaida kwenye nyumba zao,ili waweze kuanza maisha ya kawaida tena. Amesisitiza kuwa usalama unapewa kipaumbele cha kwanza katika kutekeleza yote hayo.