Mkutano kulinda mali asili kufanyika Kinshasa DRC

Mkutano kulinda mali asili kufanyika Kinshasa DRC

Umoja wa Mataifa pamoja na serikali ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo watafanya mkutano juma lijalo kujadili njia za kulinda sehemu tano zilizo kwenye orodha ya sehemu za kiasili duniani ambazo ziko kwenye hatari ya kuangamia.

Kati ya maeneo hayo matano ni pamoja na mbuga za wanyamapori za Virunga , Garamba , Kahuzi-Biega na salonga. Kutokana na habari zilitolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO ni kuwa sehemu hizo zimekabiliwa na athari zinazotokana na mizozo kwa zaidi ya miongo miwili.

Mnamo tarehe 14 mwezi huu mkutano mkuu utaandaliwa kwenye mji mkuu wa DRC Kinshasa na kuongozwa na waziri mkuu wa DRC Adolphe Muzito na katibu mkuu wa shirika la UNESCO Irina Bokova. Washiriki wakiwemo wawakilishi wa serikali , mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na wafadhili watakagua hali ya maeneo hayo na kujadili njia za kuyalinda.