Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya kisiasa Nepal bado ni tete: Landgren

Hali ya kisiasa Nepal bado ni tete: Landgren

Hali ya kisiasa Nepal bado ni ya kutia mashaka, wakati vikosi vya kulinda amani vya UM vikijiandaa kuondoka.

Hali ya kupatikana kwa utengamao wa kisiasa nchini Nepal ambayo imeshuhudia machafuko kwa miongo kadhaa ni ya kutia mashaka wakati ambapo vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa vikijiandaa kuondoka kutokana na kukoma kwa muda wake .

Vikosi hivyo vya Umoja wa Mataifa UNMIN vinatazamia kumaliza kazi zake nchini humo January 13 mwaka huu, lakini mwakilishi wa Katibu Mkuu kwenye eneo hilo Karin Landgren ameliambia baraza la usalama kuwa hakuna ishara yoyote ya matumaini ya kupatiwa ufumbuzi juu ya mizozo iliyoibuka miongo kadhaa iliyopita.

Mwakilisho huyo ametaja baadhi ya maeneo ambayo bado yanatia shaka ikiwemo pamoja na kukosekana kwa utashi wa kisiasa wa kuundwa kwa serikali mpya na kushindwa kuyaleta pamoja makundi ya waasi 19,000 ambayo yalipaswa kuingizwa kwenye mchakato wa mafungamano kufuatia makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2007.

Katika makubaliano hayo yaliyolenga kumaliza machafuko na uhasama wa kisiasa uliogharimu maisha ya watu 13, ilipendekezwa kwamba makundi yote hasimu yashirikishwe kwenye uundwaji wa serikali mpya.