Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za wapiga kura ziheshimiwe Sudan:Navi Pillay

Haki za wapiga kura ziheshimiwe Sudan:Navi Pillay

Zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya wananchi wa Sudan Kusini kuanza kupiga kura ya maoni ya kuamua hatma yao hapo siku ya Jumapili ijayo, mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameutaka uongozi wa Sudan kuhakikisha kura ya maoni inakuwa huru na ya haki.

Amesema haki za raia lazima ziheshimiewe kama anavyofafanua msemaji wa ofisi ya kamishna wa haki za binadamu Rupert Colville.

(SAUTI YA RUPERT COLVILE)

Bi Pillay ameongeza kuwa serikali ya Khartoum na ya Juba lazima zichukue mipango madhubuti ya kuzuia jaribio lolote la kuwatisha wapiga kura au kuvuruga matokeo. George Njogopa anaripoti.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)