Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ouattara amkataka Gbagbo kukubali kushinda

Ouattara amkataka Gbagbo kukubali kushinda

Mgombea wa upinzani aliyetangazwa mshindi katika uchaguzi wa Novemba mwaka jana na kuzua utata nchini Ivory Coast Alassane Ouattara amesema ana imani suluhu ya mzozo wa kisiasa nchini humo itapatikana hivi karibuni.

Akizungumza na Radio ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo,mjini Abijan UNOCI bwana Ouattara amesema matakwa ya wananchi lazima yatimizwe na walimpigia kura kwa wingi ikiwemo asilimia 60 ya wanajeshi.

Bwana Ouattara ambaye anaungwa mkono na Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa ambayo imemtambua kama mshindi halali wa duru ya pili ya uchaguzi huo wa Rais ameongeza kuwa angependelea kumaliza mvutano huo kwa njia ya amani ya majadiliano kuliko kutumia nguvu, na amemtaka bwana Laurent Gbagbo kukubali kushindwa.

(SAUTI YA ALASSANE OUATTARA)