Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Machafuko yanaendelea mjini Duekoue Magharibi mwa Ivory Coast:OCHA

Machafuko yanaendelea mjini Duekoue Magharibi mwa Ivory Coast:OCHA

Taarifa iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA inasema machafuko katika mji wa Magharibi wa Duekoue nchini Ivory Coast kati ya jamii za kikabila za Malinke na Guere yanaendelea.

Machafuko hayo yamezuka baada ya kuuawa kwa mwanamke mfanya biashara kutoka jamii ya Malinke January 3 mwaka huu. Kwa mujibu wa OCHA machafuko hayo yamesababisha ongezeko la wakimbizi wa ndani mjini hapo ambao sasa wamefikia 10,000 ikilinganishwa na 1579 siku mbili zilizopita.

Duru za habari zinasema watu zaidi ya 10 wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Nako katika mji wa Danane wakimbizi wa ndani 1061 wanahifadhiwa katika shule moja na makanisa matatu, huku wakimbizi wengine 114 wakihifadhiwa na familia mbalimbali. Tangu kuzuka machafuko nchini Ivory Coast baada ya uchaguzi wa Novemba mwaka jana mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yakitoa msaada kwa wakimbizi na waathirika ikiwemo UNHCR na UNICEF. Gaelle Bausson ni msemaji wa UNICEF.

(SAUTI YA GAELLE BAUSSON)