Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanaharakati wa ukimwi Nigeria kuongoza UNFPA

Mwanaharakati wa ukimwi Nigeria kuongoza UNFPA

Aliyekuwa waziri wa afya nchini Nigeria aliye na tajriba kuuwa katika kupambana na ugonjwa wa ukimwi amechukua uongozi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na kusaidia nchi zilizo na matatizo ya afya ya uzazi na maendeleo UNFPA.

Babatunde Osotimehin ambaye pia amehudumu kama msemaji wa afrika kuhusu masuala afya ya uzazi na watoto wachanga ni wa nne sasa kuliongoza shirika hilo.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linazisaidia nchi kwa kutumia takwimu za idadi ya watu na programu zingine kupunguza umaskini na kuhakikisha kuwa kila mimba ni salama, kila kijana haishi na virusi vya ukimwi na kila msichana na mama amepewa heshima anayostahili.

Akitangaza uteuzi huo katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema kuwa Osotimehin ana tajriba kubwa ya kuliongoza shirika hilo.