Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Shirikisho la soka Asia kupambana na njaa:FAO

Shirikisho la soka Asia kupambana na njaa:FAO

Shirikisho la soka la Asia AFC litazitoa mechi tatu za kandanda kwa ajili ya vita dhidi ya njaa na umasikini wakati wa kombe la Asia.

Mechi hizo ni za kuonyesha mshikamano, zitachezwa mjini Doha Qatar na zinaandaliwa kwa ushirikiano wa AFC na shirika la chakula na kilimo duniani FAO. Mechi ya kwanza iliyotengwa kwa vita hivyo dhidi ya njaa ni mechi ya ufunguzi wa kombe la Asia itakayochezwa Januari 7 mwaka huu kati ya Qatar na Uzbekhistan.

Mechi zingine mbili zitakazoihusisha Qatar zitakuwa ni za kampeni hiyo. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Katika mchezo wa ufunguzi utaofanyika January 7, ikizikutanisha timu za Qatar na Uzbekhistan, zingatio kubwa litakuwa ni kukabiliana na tatizo la njaa. Michezo mingine itakayofuata ambayo Qatar itakuwa dimbani suala hilo hilo la kukabili njaa litapewa kipaumbele.

Wakati wa michezo hiyo wachezaji pamoja na mashabiki wa soka watapeperusha ujumbe mmoja wa kuyataka mataifa yote duniani kuongeza nguvu kukusanya rasilimali ili kuokoa mamilioni ya watu wanaotaabika kwa njaa.

FAO inaamini kuwa hatua hiyo itafanikisha kutunisha mfuko wake unaojulikana kama TeleFood, ambao umekuwa ukifanya kazi duniani kote kwa ajili ya kuwafikia watu wenye matatizo ya njaa.