Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usalama nchini Somalia lazima uimarike:Mahiga

Usalama nchini Somalia lazima uimarike:Mahiga

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga jana amefanya ziara ya ghafla mjini Moghadishu na kukutana na Rais Sheikh Sharif Ahmed na waziri mkuu Mohamed Abdullahi Mohamed.

Katika mazungumzo yao wamejadili masuala kadhaa ikiwemo usalama na tatizo la ukame. Mahiga ameitolea wito serikali ya mpito kuimarisha hali ya usalama kwani ni muhimu kwa ajili ya nchi hiyo iliyoghubikwa na miongo miwili ya vita kuweza kusaidiwa na jumuiya ya kimataifa hasa tatizo la wakimbizi wa ndani.

Mahiga na uongozi huo wa serikali ya mpito pia wamejadili athari za ukame ulioathiri maelfu ya watu katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo na hasa Kusini na Katikati mwa nchi.

Wamejadili jinsi gani serikali itakavyojitahidi kuwasaidia waathirika walio katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi la wanamgambo wa Al Shabaab ambako serikali ya mpito haiwezi kuingia.

(SAUTI YA AUGUSTINE MAHIGA)