UNEP imezindua program ya masuala ya mazingira Haiti

5 Januari 2011

Mpango wenye kutia matumaini ya kufufua mazingira na maendeleo endelevu Kusini Magharibi mwa Haiti umezinduliwa jana na shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP mjini Port-Salut.

Mpango huo umezinduliwa kwa ushirikiano na wadau wengine ikiwemo serikali ya Haiti, serikali ya Norway, huduma za msaada za kanisa Katoliki, taasisi ya masuala ya dunia ya chuo kikuu cha Columbia na mashirika mbalimbali yasisyo ya kiserikali ya Haiti. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Programu hii ijulikanayo kama Cote Sud na ambayo itachukua muda wa miaka 20 kutekelezwa inalenga kuchangia maendeleo katika nchi Kavu na sehemu zilizo na maji zenya ukubwa wa kilomita 1280 mraba. Jamii kumi zilizo na idadi ya watu wanaokadiriwa kuwa 205,000 zitanufaika moja kwa moja kutokana na mpango huu ambao utahusisha masuala kama upanzi wa miti, kuzuia mmomonyoko wa udongo, kilimo cha samaki, biashara ndogo ndogo na pia kuhakikisha kuwepo kwa maji , huduma za afya na elimu.

Katibu katika shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP Achim Steiner amesema mkuwa kuboresha mazingira katika eneo hilo la kusini magharibi mwa Haiti itakuwa hatua kubwa kwa maendeleo ya muda mrefu kwa wenyeji .

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter