Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vyombo vya habari vya serikali Ivory Coast vyaiandama UNOCI

Vyombo vya habari vya serikali Ivory Coast vyaiandama UNOCI

Wafuasi na kambi ya Rais Laurent Gbagbo kupitia radio na televisheni ya serikali ya Ivory Coast RTI, wameanza duru ya pili ya kampeni za chuki dhidi ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNOCI.

Kampeni hizo imebainika kuwa zilipangwa na kambi ya Bwana Gbagbo tangu Decsemba 29 mwaka jana. Tangu wakati huo TRI imeendelea kuonyesha picha za watu wawili waliojeruhiwa kwa risasi wakati wa doria ya mpango wa UNOCI eneo la Abobo.

Kampeni za chuki zimeongezeka kwenye kambi ya Gbagbo, nah ii ni mara ya pili kambi ya Rais Gbagbo inafanya kampeni mbaya na za kuchafua jina dhidi ya UNOCI. UNOCI imetoa wito wa kusitishwa mara moja kampeni hizo. Na imeendelea kukanusha vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu kama inavyodai kambi ya Gbagbo.