Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makao makuu ya Ouattara yambuliwa Ivory Coast:UM

Makao makuu ya Ouattara yambuliwa Ivory Coast:UM

Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast unathibitisha taarifa kwamba makao makuu ya kiongozi wa upinzani Alassane Ouattara yameshambuliwa mjini abijan Ivory Coast.

Inadhaniwa kwamba majeshi yanayomuunga mkono Rais Laurent Gbagbo yamefanya mashambulio hayo Jumatatu asubuhi. Bwana Gbagbo anagoma kumuachia madaraka bwana Ouattara ambaye jumuiya ya Kkimataifa inamtambua kama mshindi wa uchaguzi.

Hamadoun Toure kutoka mpango wa Umoja wa Mataifa Ivory Coast anasema watu wawili wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa. "Makao makuu ya Ouattara watu wamekamatwa, hatuna uthibitisho wa mauaji lakini kwa taarifa zisizothibitishwa watu wawili wameuawa."