Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Karin Landgren mjumbe mpya wa UM Burundi:Ban

Karin Landgren mjumbe mpya wa UM Burundi:Ban

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Karin Landgren kutoka Sweden kama mjumbe wake maalum nchini Burundi ambapo ataongoza oparesheni za Umoja wa Mataifa za kulisaidia taiafa hilo kupiga hatua za kuwa na amani na za kimaendeleo.

Bi Landgren anachukua mahala pa Charles Petrie mwakilishi maalum wa katibu mkuu nchini Burundi. Afisi hiyo pia iliyo na mda wa kuhudumu wa miezi 12 kuanzia hapo hapo kesho ina jukumu la kuisaidia serikali katika jitihada zake za kuimarisha sekta muhimu hususan mahakama na bunge, kupambana na ukwepaji wa sheria na kulinda haki za binadamu.

Hii ni moja kati ya oparesheni za hivu majuzi za Umoja wa Mataifa nchini Burundi ambapo maelfu ya watu waliuawa kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya wahutu nba watusi hata kabla ya nchi hiyo kupata uhuru wake kutoka kwa Ubelgiji mwaka 1962.