Skip to main content

Ban amelaani vikali shambulizi kanisani nchini Misri

Ban amelaani vikali shambulizi kanisani nchini Misri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amelaani vikali tukio la shambulizi la bomu lililowauwawa watu 21 na kuwajeruhi wengine 70 wakati wakiwa kwenye ibada ya mkesha wa mwaka mpya kwenye kanisa Qiddissin Coptic mjini Alexandria, Misri.

Ban amesema kuwa ameshtushwa mno na tukio hilo na amehaidi kuwa nyuma ya serikali ya Misiri inayoendesha juhudi za kuwasa wahalifu hao.

Pia ametuma salama zake za rambirambi kwa ndugu na familia waliofikwa na msiba huo na kuwatakia nafuu ya haraka waliojeruhiwa.