Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wa Kiafrika wazama baharini wakielekea Yemen

Wahamiaji wa Kiafrika wazama baharini wakielekea Yemen

Wahamiaji zaidi ya 40 wa Kiethiopia na Kisomali wamezama kwenye mwambao wa Yemen baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama kwenye Ghuba ya Aden.

Kwa mujibu wa mashirika ya misaada katika eneo hilo boti nyingine yenye idadi isiyiojulikana ya wahamiaji haijulikani ilipo. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema wanaume watano kati ya abiria 46 wa Ethiopia na Somalia wamenusurika katika mkasa huo. Jean-Philippe Chauzy kutoka shirika la kimataifa la uhamiji IOM anasema vifo vya wahamiaji hao ni kitendo cha kujutia.

(SAUTI YA JEAN-PHILIPPE CHAUZY)

Ameongeza kuwa umasikini uliokithiri, matatizo ya kiuchumi na kisiasa katika pembe ya Afrika yamekuwa yakiwashinikiza wahamiaji kuwalipa wasafirishaji haramu kiwango kikubwa cha fedha na kufanya safari hiyo ya hatari kuvuka bahari.