Wakimbizi wa Ivory Coast wazidi 20,000: UNHCR
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR leo limesema limeorodhesha wakimbizi zaidi ya 20,00 wa Ivory Coast waliokimbia nchi jirani ya Liberia tangu kuzuka machafuko ya baada ya uchaguzi mwezi Novemba mwaka jana.
Kwa mujibu wa msemaji wa UNHCR Babar Bloch wakimbizi hao bado wanaendelea kuingia Liberia kwa idadi ya 400 hadi 500kwa siku. Amesema wakimbizi wengine 222 wamekimbilia Guinea huku 19 wakiomba hifadhi nchini Ghana.
UNHCR inasema wengi wa wanaokimbia ni wanawake na watoto. Watu 179 wameuawa katika machafuko ya kisiasa nchini Ivory Coast tangu mwezi Novemba na imekuwa vigumu kufanya uchunguzi limesema shirika hilo.