Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matakwa ya watu wa Ivory Coast lazima yaheshimiwe:Ban

Matakwa ya watu wa Ivory Coast lazima yaheshimiwe:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amerejea kusistiza msimamo wa Umoja wa Mataifa kwamba matokeo ya uchaguzi wa karibuni wa Urais nchini Ivory yanadhihirisha matakwa ya watu na hivyo matokeo lazima yaheshimiwe.

Katika mazungumzo kwa njia ya simu na Rais aliyechaguliwa Alassane Ouattara, Bwana Ban amesisitiza kwamba jumuiya ya kimataifa imejidhatiti kufanya kazi pamoja ili kumaliza mtafaruku wa kisiasa kwa njia ya amani katika taifa hilo la Afrika ya Magharibi.

Icory Coast imeingia katika mvutano wa kisiasa baada ya Rais Laurent Gbagbo kukataa matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi mpinzani wake bwana Ouattara, katika duru ya pili ya uchaguzi tarehe 28 November mwaka jana.Jumuiya ya kimataifa inamtambua bwana Ouattara kama rais aliyechaguliwa nchini humo.

Katibu Mkuu amemwambia Rais Ouattara kwamba anatiwa hofu na taarifa za ukiukaji wa haki mza binadamu na kuongeza kwamba majeshi ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini humo UNOCI yamepewa maagizo ya kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha yanapata fursa ya kuingia maeneo yaliyoathirika ili kuzuia na kuchunguza visa vya ukiukaji wa haki za binadamu ili wahusika waweze kuwajibishwa.

Bwana Ban pia ametilia maanani wito wa Bwana Ouattara wakati wa mazungumzo yao wa kutaka mahakama mya kimataifa ya ICC kufanya uchunguzi wa mapema