Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa kusaidia kudumisha lugha ya Kiswahili Kenya

Umoja wa Mataifa kusaidia kudumisha lugha ya Kiswahili Kenya

Chuo kikuu cha Nairobi nchini Kenya kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa kupitia ofisi yake iliyoko Nairobi UNON wamezindua rasmi programu ya kwanza kabisa ya shahada ya uzamili katika ufasiri na kutafsiri katika kanda ya Afrika ya Mashariki.

Uzinduzi huo uliofanyika Novemba mwaka huu kwenye chuo kikuu cha Nairobi na kupewa jina la "Mradi wa Afrika" ambao umefanikiwa kwa kujumisha juhudi za wadau mbalimbali vikiwemo vyuo vikuu vingine barani Afrika, taasisi za muungano wa Ulaya, Bank ya maendeleo ya Afrika, muungano wa Afrika, mashirika mengine ya kikanda ya Afrika na Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa mradi huo umetokana na kutambua kwamba katika kipi9ndi cha miaka mine ijayo mashirika ya kimataifa yatapoteza asilia 40 ya wataalamu wake wa lugha kutokana na kustaafu na Afrika ndio itakayoguswa pakubwa kutokana na ukosefu wa wataalamu waliobbobea katika lugha.

Mradi huo unaojumuisha lugha nyingi , Kiswahili kikipewa kipaumbele unaonekana kama mfano mzuri kwa vyuo vikuu vingine kuiga barani afrika.

Kuna baadhi ya nchi ambazo tayari zimeanza kufuata nyayo za mfumo huo ikiwemo Msumbiji kwa kuanzisha program katika chuo kikuu cha Mozambique mjini Maputo na na Afrika ya Kusini katika chuo kikuu cha Mandela Metropolitan kilichopo mjini port Elizabeth.

Mwandishi wetu Jason Nyakundi amekwenda kwenye chuo kikuu cha Nairobi na kuzungumza na baadi ya wahadhiri na mmoja wa wanafunzi wa shahada hiyo ya uzamili ya ufasiri na tafsiri ya lugha ya Kiswahili.

(PKG YA JASON NYAKUNDI)