Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za Tanzania kupunguza vifo vya watoto zakabiliwa na changamoto

Juhudi za Tanzania kupunguza vifo vya watoto zakabiliwa na changamoto

Juhudi za Tanzania katika kufikia lengo la maendeleo la milenia namba nne, kupunguza vifo vya watoto wachanga kabla ya mwaka 2015 zinakabiliwa na changamoto.

Tatizo la vifo vya watoto wa umri wa miaka mitano ni mtihani kwa nchi nyingi duniani, bara la afrika likiongoza na kufanya lengo hilo kuwa changamoto kubwa katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.

Tanzania ni moja ya nchi duniani zilizo na rekodi kubwa ya idadi ya vifo vya watoto wachanga, na kwa sasa imeamua kulivalia njuga suala hilo, lakini hata bado inakabiliwa na vikwazo. Mwandishi wetu wa Dar es salaam Tanzania George Njogopa amedadisi sababu na juhudi zinazofanyika katika makala hii. Ungana naye katika makala hii.

(MAKALA NA GEORGE NJOGOPA)