Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uchumi wa dunia utakuwa kwa wastan mwaka 2011:IMF

Uchumi wa dunia utakuwa kwa wastan mwaka 2011:IMF

Hali ya uchumi wa dunia inatazamia kukua kwa wastani mwaka ujao, lakini pia nchi za Ulaya zitakabiliwa na changamoto ya ulipaji madeni ili kudhihirisha ukuaji wa uchumi huo.

Shirika hilo la fedha limesema kuwa ukoaji wa uchumi unatazamiwa kuwa wa wastani katika mataifa yaliyoendelea hali ambayo pia itashuhudiwa kwa mataifaifa yanayoinukia kiuchumi.

Hata hivyo IFM imeonya kuwa ongezeko hilo la uchumi pengine lisiweza kupata mabadiliko halisi kama nchi za Ulaya zitashindwa kukabiliana na changamoto ya ulipaji mikopo.

Kwa mujibu wa mchumi mwandamizi wa shirika hilo Olivier Blanchard amesema maeneo ya ukosefu wa ajira na kuanguka kwa masoko yanaweza kuanza kupata kasi mpya ya mafanikio.