Watu walioathirika na mafuriko Pakistan bado wanahitaji msaada: UM

31 Disemba 2010

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Pakistan balozi Rauf Engin Soysal na mratibu wa Umoja wa Mataifa nchini Pakistan Tomo Pakkala inasema mamilioni ya wapakistan bado wanahitaji msaada kukabili athari za mafuriko yaliyowakumba.

Mafuriko hayo ya yalisababisha mtafaruku mkubwa wa kibinadamu kuwahi kuikumba Pakistan na kuathiri watu takribani milioni 20. Maafisa hao wamesema kwa nia walionayo watu wa Pakistan, kwa msaada wa kitaifa na Kimataifa nchi hiyo itazishinda changamoto za mafuriko hayo.

Wameongeza kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuwasaidia watu wa Pakistan watakapohitaji msaada kupitia miradi na mipango yake mbalimbali.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter