WFP yakaribisha mchango wa kihistoria wa Brazil katika kupambana na njaa

31 Disemba 2010

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP leo limekaribisha msaada mkubwa kabisa kuwahi kuupata kutoka nchini Brazili .

Msaada huo utaisukumua nchi ya Brazili kuwa miongoni mwa orodha ya wachangiaji kumi bora wa WFP na kudhihirisha juhudi za Brazili za kupambana na njaa nyumbani na kimataifa.

Mkurugenzi mkuu wa WFP Josette Sheeran amesema tunaishukuru serikali ya Brazil kwa msaada wake ambao utatuwezesha kulisha mamilioni ya watu wanaokabiliwa na njaa duniani. Ameongeza kuwa chini ya uongozi wa Rai Inacio Lula Da Silva Brazil inakuwa miongoni mwa wahisani wanaoongoza vita dhidi ya njaa duniani.

Brazili imethibitisha msaada wa tani nusu milioni za chakula ambacho kitawalisha watu waliokubwa na majanga ya asili, dharura na majanga mengine hususan Afrika na Amerika Kusini.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter