Watu wa Sili hatimaye kulinda na sheria Congo-Brazzaville:UNICEF

31 Disemba 2010

Kuanzia tarehe 30 Desemba mwaka huu wa 2010 watoto wa nchi ya Congo Brazzaville kutoka jamii ya watu wa asili watapata fursa za masuala ya afya, elimu na kulindwa kutokana na kuwekwa sheria za kuwalinda.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto nchini humo UNICEF Marianne Flach, sheria hiyo ni ya kipekee katika kanda hiyo na inaweka mfano kwa nchi zingine zilizo na watu wa asili kuchukua hatua kama za Congo kuilinda jamii hiyo.

Ameongeza kuwa kuanza kutekelezwa kwa sheria hiyo ni hatua kubwa kwa historia ya taifa la Congo. Seneti ya nchi hiyo ilipitisha sheria ya kuchagiza na kulinda haki za jamii ya watu wa asili baada ya bunge la taifa kuidhinisha kutokana na mapendekezo ya kamati ya kimataifa ya haki za watoto katika kutekeleza mkataba wa haki za watoto wa mwaka 1993 ambao nchi hiyo iliuridhia.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter