Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waliokumbwa na mafuriko Colombia kusaidiwa na UM

Waliokumbwa na mafuriko Colombia kusaidiwa na UM

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na masuala ya majanga wameongeza nguvu kusaidia shughuli za uimarishaji hali ya maisha kwa mamia ya wananchi wa Colombia ambao wameathiriwa vibaya na mafuriko.

Timu hiyo ya wataalamu iliyowasili mwanzoni mwa wiki hii, inatazamiwa kuwepo nchini humo kwa muda wa wiki tatu kusaidia shughuli za uratibu na usimamizi wa shughuli nyingine. Mvua kubwa inayoendelea kunyesha ikiambatana na La Niña imeleta maafa makubwa kwa wananchi wa Colombia.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya kiutu OCHA limesema kuwa maeneo mengi ikiwemo yale ya pwani ya Caribbean yameathiriwa na mafuriko hayo.